Serikali ya Somalia imeongeza operesheni za kijeshi dhidi ya kundi la Al-Shabab katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Operesheni hizo zinafanywa kwa ushirikiano na vikosi vya kimataifa vikiwemo vya AUSSOM pamoja na washirika wengine wa kimataifa.
Kundi la Al-Shabab limekuwa likifanya mashambulizi dhidi ya serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 16, likilenga vikosi vya usalama, maafisa wa serikali na raia.
CHANZO: Newstimetr














