Katibu wa Hazina wa Uganda Ramathan Ggoobi amesema uchumi wa nchi hiyo unaendelea kuwa imara licha ya changamoto za ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo, amekiri kuwa bado kuna udhaifu katika mfumo wa ukusanyaji wa mapato ambao unazuia maendeleo ya kiuchumi kufikia kiwango kinachotarajiwa.
Alisema kuwa akaunti ya fedha ya Uganda imeonyesha mafanikio baada ya kurekodi mapato ya dola bilioni 5.6, huku uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni ukifikia dola bilioni 3.56.
Ggoobi aliongeza kuwa salio la malipo ya kimataifa lilisajili ziada ya dola bilioni 2.37, hali inayoonyesha kuwa fedha nyingi zaidi zimeingia nchini kuliko kutoka.
CHANZO: Newstimetr














