Sudan yarejea tena IGAD baada ya kuwa nje kwa miaka miwili

Uamuzi wa kurejea IGAD, unafuatia kikao cha mwezi Januari kati ya Katibu Mtendaji wa IGAD, Workneh Gebeyehu, na Waziri Mkuu wa Sudan, Kamil Idris.

Newstimehub

Newstimehub

9 Februari, 2026

d19b24031a8096ac5d96d4f6d776a4c34f620742823cbafa4b4dd94dfb794a24

Sudan imetangaza kurejea ndani ya Umoja wa IGAD, miaka miwili baada ya kusitisha uanachama wake, kufuatia uamuzi wa kumkaribisha kiongozi wa wanamgambo, Mohamed Hamdan Daglo kwenye kikao mojawapo cha umoja huo.

 “Serikali ya Sudan inarudisha uanachama wake ndani ya IGAD,” ilisema serikali ya nchi kupitia taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje.

Mwezi Januari 2024, Sudan ilisitisha uanachama wake IGAD, baada ya IGAD kumkaribisha kiongozi wa RSF katika kikao nchini Uganda.

Kikundi cha RSF kimekuwa kwenye mgogoro na jeshi la Sudan tangu Aprili 2023, katika mgogoro ulioua maelfu ya watu na kuwaancha wengine milioni 11 bila makazi.

Uamuzi wa kurejea IGAD, unafuatia kikao cha mwezi Januari kati ya Katibu Mtendaji wa IGAD, Workneh Gebeyehu, na Waziri Mkuu wa Sudan,  Kamil Idris.