Bobi Wine: Mimi si mhalifu

Akizungumzia tishio kutoka kwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo na mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, Wine alisema:“Mimi si mhalifu bali mgombea Urais na sio hatia kugombea dhidi ya baba yake.”

Newstimehub

Newstimehub

21 Januari, 2026

6af9663eb4e4a68e58f0f9dcddd0373979e3bb005927aa81975bb5b001d40676

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amesema kuwa yeye si mhalifu, baada ya kukimbilia mafichoni kufuatia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa wiki iliyopita nchini humo.

Wine, mwenye umri wa miaka 43, anadaiwa kukimbilia kusikojukulikana, baada ya makazi yake kuvamiwa.

Wine, ambaye aliuita uchaguzi wa Alhamisi iliyopita kama “wizi wa waziwazi”,  amesema kuwa ameendelea kuwa mafichoni, akiwa ulinzi na watu wa ‘kawaida sana’.

Akizungumzia tishio kutoka kwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo na mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, Wine alisema:

“Mimi si mhalifu bali mgombea Urais na sio hatia kugombea dhidi ya baba yake.”

Siku ya Jumanne, Kainerugaba, alionesha matamanio yake ya kumrithi baba yake, akiweka wazi azma yake ya kuuondoa uhai wa Wine, kupitia ukurasa wa X.

“Tumeua magaidi 22 wa NUP toka wiki iliyopita,” aliandika Kainerugaba.

“Ninaomba wa 23 awe Kabobi.”