Mzimu wa Shakahola wazuka tena Kenya, miili 32 imefukuliwa.

Miili 32 imefukuliwa wiki hii katika kijiji cha Kwa Binzaro, karibu na Shakahola, Kaunti ya Kilifi nchini Kenya.

Newstimehub

Newstimehub

29 Agosti, 2025

7f9779d2fdecf975f281afb5bcc6a9e9787e02aa7c3e105a85ef0c463bfbf9af

Mauaji hayo yanahusishwa na imani potofu ya kufunga hadi kufa inayohusishwa na mhubiri Paul Mackenzie wa kanisa la Good News International.

Dkt. Richard Njoroge, daktari wa serikali anayesimamia uchunguzi huo, amesema zoezi la ufukuaji limeanza wiki iliyopita na hadi sasa jumla ya miili 32 imepatikana.

Tukio hili linafufua maumivu ya vifo vya Shakahola mwaka 2023, ambapo watu zaidi ya 400 walifariki kwa njaa wakifuata mafundisho ya “mwisho wa dunia.”