Mzize ‘Goal Machine’: Mshambulizi mwenye ari kubwa aliyelenga macho kwa ubingwa wa CHAN

Kwa Tanzania, ulikuwa ni zaidi ya ushindi—ulikuwa ushindi wa tatu mfululizo wa hatua ya makundi na tikiti ya kihistoria ya kutinga hatua ya robo fainali ya Mashindano ya TotalEnergies African Nations Championship (CHAN) 2024.

Newstimehub

Newstimehub

12 Agosti, 2025

a157f96e772bffd9b09b0872dd9d8eeb10b2d5a42c095f0d8ab67477a41e5bdd

Tangu kulia kipenga cha kuanza mechi, uwanja ulitetema kwa kishindo cha Clement Francis Mzize.

Mshambuliaji huyo alikimbia, alidodosa na alichenga, huku macho yake yakilenga kutikisa wavu wa adui.

lakini Mzize hakufunga tu – aliunguruma, na kutoa mabao mawili ndani ya dakika 20 na kuizamisha Madagascar na kuupeleka Uwanja wa Benjamin Mkapa kupasuka kwa sauti za mashabiki waliojawa furaha tele. Kwa mashabiki wa Madagascar, iwapo hawakujua, hiyo tayari ilikuwa dalili kuwa Tanzania ni moto wa kuotea mbali.

Hadi kufikia mwisho wa usiku, ubao wa matokeo ulisomeka 2-1 kwa wenyeji, na Mzize alikuwa ametawazwa kuwa mchezaji bora wa mechi wa TotalEnergies.

Zaidi ya Ushindi

“Namshukuru Mungu kwa nafasi hii ya kuwa katika nafasi hii na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi,’’ alisema Mzize. ‘‘Ni vyema tukaendelea kusonga mbele katika mashindano hayo, na tunatumai kufika mbali katika michuano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies 2024.” Aliwaambia waandishi wa habari baada ya mechi.

81d3925b5b1f2236e5613c33b508835e860aba9e58a491a99bc8cd502c4854c5 1

Kwa Tanzania, ulikuwa ni zaidi ya ushindi—ulikuwa ushindi wa tatu mfululizo wa hatua ya makundi na tikiti ya kihistoria ya kutinga hatua ya mtoano ya Mashindano ya TotalEnergies African Nations Championship (CHAN) 2024.