Zanzibar kuagiza mchanga kutoka Tanzania bara
Serikali ya Zanzibar imetangaza mpango wa kuanza kununua mchanga kutoka Tanzania Bara kwa ajili ya kutumika katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa visiwani humo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Zanzibar, Nadir Abdul Latif, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya siku 100 za uongozi wa Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi, katika kipindi cha pili cha uongozi wake.
kubwa ya maendeleo inayotekelezwa Zanzibar kwa sasa inahitaji kiasi kikubwa sana cha mchanga. Kutokana na hali hiyo, serikali imefanya tathmini na kuona ni vyema kuanza kuagiza mchanga kutoka Tanzania Bara kwa ajili ya miradi hiyo mikubwa,” amesema.
Chanzo: Newstimetr














