Takriban 1,000 waliuawa katika maporomoko ya ardhi yaliyoharibu kijiji katika eneo la Milima ya Marra magharibi mwa Sudan, na kuacha mtu mmoja tu aliyenusurika, The Sudan Liberation Movement/Army ilisema Jumatatu.
Maporomoko ya ardhi yalitokea Agosti 31 baada ya siku kadhaa za mvua kunyesha, kundi linaloongozwa na Abdelwahid Mohamed Nour lilisema katika taarifa.
Vuguvugu hilo linalodhibiti eneo lililoko katika jimbo la Darfur, lilitoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya misaada kusaidia kurejesha miili ya wahanga wakiwemo wanaume, wanawake na watoto.