Ni mtu mmoja pekee aliyenusurika na janga hilo katika kijiji cha Tarseen katika eneo la milima la Jebel Marra katika eneo la Darfur, lilisema kundi la ‘Sudan Liberation Movement/A (SLM/A).
SLM/A, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikidhibiti na kutawala sehemu iya Jebel Marra, ilitoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya misaada kusaidia kukusanya miili ya walioathiriwa, ikiwa ni pamoja na miili ya wanaume, wanawake na watoto.
“Tarseen, maarufu kwa uzalishaji wake wa machungwa, sasa imeharibiwa kabisa,” kikundi hicho kilisema katika taarifa.