Waziri Mkuu wa Ethiopia adai madini ya nchi hiyo yamekuwa yakipotea kupitia Mto Nile

Ethiopia inasema itazindua hivi karibuni bwawa lake kuu, limejengwa kwenye Mto Nile na Serikali inasema lina na uwezo wa kuzalisha megawati 6000 ya umeme ikikamilika

Newstimehub

Newstimehub

2 Septemba, 2025

353967ca1b6097e6950ef14685b83350b9388d7cba389b526904ef85b126d4e9

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema Mto Nile wa Ethiopia yaani Blue Nile, ambao hutoa hadi asilimia 86 ya maji ya Nile, kwa karne nyingi umechukua sio tu ardhi yenye rutuba ya nchi hiyo lakini pia dhahabu yake, na kuiacha Ethiopia bila faida.

Katika hotuba yake kupitia runinga Jumatatu usiku, siku chache kabla ya uzinduzi unaotarajiwa wa Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD), Abiy alifichua kuwa katika uchimbaji kwenye bwawa hilo kulipatikana “mabaki ya dhahabu kwenye mchanga uliokusanywa.”

“Hii inazidisha majuto kwamba Mto Nile umekuwa ukichukua sio ardhi yetu tu, bali pia dhahabu ya Ethiopia kutoka kwenye milima yetu,” Waziri Mkuu Ahmed alisema.

887b002fb576f76950c7f4d750c739f7dffec63ba3a60aa8bed80278681d934e 1

Waziri Mkuu aliongeza kuwa Ethiopia imepata kutambuliwa kwa kiasi kidogo sana kwa kulinda utajiri wake wa asili.

“Sijawahi kusikia mtu akisema, ‘Uishi maisha marefu, miaka yako iwe mingi, kwa sababu yako tumepata haya,’ baada ya udongo wetu, dhahabu, samaki, magogo na miti yetu kuchukuliwa, badala yake, tulichosikia ni hasira na dharau kwamba tunatetea na kulinda mali zetu,” alisema.

Ethiopia imekuwa na mvutano na Misri kwa ujenzi wa bwawa lenye ukubwa wa megawati 6000, huku Misri ikisisitiza kuwa maji ya Mto Nile hayafai kutumika kwani mtiririko kwenda kwake utapungua.

Misri inategemea maji ya Mto Nile kwa kilimo na matumizi na inashikilia maamuzi yaliyofanywa na Uingereza wakati wa ukoloni.