Watu wasiopungua 25 wamefukiwa kwenye mgodi mmoja kaskazini mwa Tanzania

Juhudi za uokoaji zinaendelea katika mgodi mmoja nchini Tanzania baada ya watu wasiopungua 25 kufukiwa, Rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan alisema siku ya Alhamisi.

Newstimehub

Newstimehub

14 Agosti, 2025

91c6dc42d20ec2e1a539b6e4cd5a084ef8ca8314f799b62e7fa6315e86608adc

Juhudi za uokoaji zinaendelea katika mgodi mmoja nchini Tanzania uliotititia siku tatu zilizopita, na kuwafukia watu wasiopungua 25, Rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan alisema siku ya Alhamisi.

Ajali hiyo ya Jumatatu ilitokea wakati ukarabati ukiendelea katika mgodi wa Nyandolwa Mkoa wa kaskazini magharibi wa Shinyanga, karibu kilomita 200 kaskazini mwa mji mkuu, Dodoma.

Katika taarifa kwenye mtandao wa X, Rais Samia alisema “Ndugu zetu 25 waliokuwa wakifanya kazi kwenye mgodi wallifukiwa na kifusi.”

Alielezea “masikitiko yake makubwa” kuhusu ajali hiyo, na kusema kuwa vikosi vya ulinzi na usalama vitasaidia katika shughuli za uokoaji “kuharakisha operesheni inayoendelea.”

Ajali mbaya