Bedatu Hirpa wa Ethiopia alimshinda mwenzake Dera Dida kwa sekunde nne na kushinda mbio za wanawake katika mbio za Paris Marathon, huku Mkenya Benard Biwott akiambulia ushindi katika mbio za wanaume, akimaliza sekunde 48 kabla ya mshindani wake wa karibu siku ya Jumapili.
Hirpa, ambaye alimshinda Dida katika kumaliza kwa karibu katika mbio za Januari za Dubai Marathon pia, alimaliza mbio za Jumapili kwa saa mbili, dakika 20 na sekunde 45 huku mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25 akiwa kwenye kundi la mbele na wengine ikiwa imebaki kilomita tano za mwisho huku Dida pekee akiwa na muelekeo mzuri.
Biwott pia aliwaacha wengine nyuma ikiwa imebaki kilomita 10 za mwisho, akimaliza kwa saa mbili, dakika tano na sekunde 25, mbele ya Ibrahim Hassan wa Djibouti, ambaye alikuwa wa pili katika mbio hizo za wanaume.
Mkenya Sila Kiptoo aliyekuwa sekunde nane nyuma ya Hassan, alimaliza wa tatu katika mbio za hizo huku Angela Tanui pia kutoka Kenya akishika nafasi ya tatu kwa upande wa wanawake akimaliza sekunde 18 baada ya Dida.