Wafanyakazi watano wa kujitolea wauawa Sudan wakiwa wanasambaza chakula, kulingana na IFRC

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) limesema Jumanne kuwa wafanyakazi wake watano wa kujitolea wameuawa Sudan.

Newstimehub

Newstimehub

28 Oktoba, 2025

96b14b734f57a37e205bd024f020db090aa17fd32abde4af783c34fca5ed1db2

Wafanyakazi hao watano wameuawa katika jiji la Bara wakiwa wanagawanya chakula na wakiwa wamevaa vazi rasmi la shirika hilo, lisema IFRC, bila kutoa maelezo ya jinsi walivyouwawa au kumtaja yeyote aliyehusika.

Shirika hilo pia limesema wafanyakazi wengine watatu hawajulikani walipo.

Jeshi la Sudan na kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF) wamekuwa wakipigana tangu Aprili 2023, mapigano ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 20,000 na kuwafurusha watu milioni 14, kulingana na Umoja wa Mataifa na mamlaka za ndani.