Waasi wa M23 wauteka tena mji wa mashariki mwa DRC huku mazungumzo ya amani yakikwama

Waasi wa M23 wameuteka tena mji wa Shoa katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC baada ya mapigano na vikosi vinavyounga mkono serikali, wakaazi walisema Jumapili.

Newstimehub

Newstimehub

8 Septemba, 2025

41e0d78446af4f584f7a2842a2a55a3e7f6387afef4c7730a28d03a0ccfa4703 main 1

Waasi wa M23 siku ya Jumapili walirejea na kuuteka tena mji wa Shoa katika jimbo la Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya mapigano na vikosi vinavyounga mkono serikali, wakaazi walisema.

Shoa, iliyoko katika eneo la Masisi, ilikuwa kwa muda mfupi chini ya udhibiti wa jeshi la Kongo na wanamgambo washirika wa Wazalendo siku ya Jumamosi kabla ya waasi kurudi na kushambulia tena.

“Sasa tuko chini ya mamlaka ya waasi wa M23, ambao walishambulia mapema Jumapili hii na kuwafukuza Wazalendo waliokuwa hapa tangu Jumamosi,” alisema mkazi mmoja, Steven Bwema, alipoongea na shirika la habari la Anadolu.

Eneo hilo lilikuwa tulivu Jumapili baada ya mapigano makali yaliyotokea siku iliyotangulia.

Eneo lenye utajiri wa madini

Masisi limekuwa eneo la mzozo kwa zaidi ya miezi mitatu huku waasi na wapiganaji wanaounga mkono serikali wakigombea udhibiti. Eneo hili lina utajiri wa dhahabu, cobalt, na tantalum.