Uwanja wa ndege wa Entebbe waweka rekodi ya abiria wengi zaidi

Uwanja wa Kimataifa wa Entebbe nchini Uganda umepata abiria wengi zaidi mwezi Julai 2025 ikiwa ni 230,577, idadi kubwa zaidi katika historia ya uwanja huo wa ndege.

Newstimehub

Newstimehub

26 Agosti, 2025

d78ae73b7fa15fb283a44de422bd711d61fb363fdcdc8330edec2d3542a93756

Hii inajumuisha abiria 119,127 waliowasili na wengine 111,450 waliosafiri kutoka uwanja huo, ikiwa ni wastani wa abiria 7,437 kwa siku.

Abiria waliowasili walikuwa zaidi ya wale walioondoka katika kipindi cha mwezi huo.

Kabla ya mwezi huu mwezi mwingine ambao uwanja wa Entebbe ulipata abiria wengi ulikuwa Disemba 2024. Abiria walikuwa 222,301, ikiwa ni wastani wa abiria wanaowasili na wanaoondoka 7,171 kwa siku.