Uganda yapiga marufuku vuvuzela na firimbi wakati wa michuano ya CHAN 2024

Polisi pia wamepiga marufuku mashabiki kuingia uwanjani na vitu kama nyundo, miamvuli, mifuko mikubwa kamera za video na chupa za chai.

Newstimehub

Newstimehub

8 Agosti, 2025

63786ece4f5d69d428778def214451dd236fa452af7fe97c890dc2a09060f7b0

Huduma ya Polisi nchini Uganda imetoa masharti mapya kwa mashabiki wakati wa michuano ya kikanda ya soka ya CHAN 2024 ambayo inafanyika katika uwanja wa Taifa wa Mandela , namboole nchini humo.

“ Ili kuhakikisha matumizi salama na ya kufurahisha kwa kila mtu, bidhaa zifuatazo haziruhusiwi kabisa ndani ya majengo ya uwanja: vuvuzela, filimbi, chupa za glasi, na makopo na fataki.” imesema katika taarifa.

Inasema kuwa ilifanya mkutano wa pamoja na kamati ya kuandaa michuano hiyo nchini, na wawakilishi wa shirkisho la soka la CAF, kwa ajili ya kuimarisha usalama kwa michezo zilizosalia.