Uganda yakubali kupokea wahamiaji walionyimwa kuingia nchini Marekani

Mpango huo unahusisha watu wenye rekodi za uhalifu, watoto wasio na walezi, na wale wanaosita kurudi makwao, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo.

Newstimehub

Newstimehub

21 Agosti, 2025

e555234f549cd700fb72cbcd18e9276149f9c5cabeef8ffc671f21ab7591ac6b

Serikali ya Uganda imeafikiana na Marekani makubaliano ya kuwapokea na kuwapa hifadhi wahamiaji walionyimwa kuingia Marekani.

Kulingana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Uganda Bagiire Vincent Waiswa, mpango huo utahusisha kuwapokea wahamiaji wenye rekodi za uhalifu, watoto wasio na walezi, na wale wanaosita kurudi makwao.

 Waiswa aliongeza kuwa, nchi hizo ziko mbioni kukamilisha mpango na makubaliano hayo.