Uganda yakabiliwa na ongozeko la wakimbizi, Umoja wa Mataifa waonya

Wastani wa watu 600 kwa siku, waliingia nchini Uganda toka kuanza kwa mwaka 2025, huku idadi hiyo ikikadiriwa kufikia milioni 2, ifikapo mwisho wa mwaka.

Newstimehub

Newstimehub

4 Agosti, 2025

bc5eb80f95c41a23365378e547e8a698317465e1426b78c964c0414bb5870172

Uganda iko katika hatari ya kupokea wakimbizi milioni, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), limeonya.

Katika taarifa yake ya Jumatatu, UNHCR ilisema kuwa taifa hilo lipo katika hatari ya kupokea wakimbizi wapatao milioni 2, ifikapo mwisho wa mwaka 2025, wengi wakitokea maeneo yaliyokumbwa na machafuko ya kisiasa, ikiwemo Sudan Kusini, Sudan na DRC.

“Toka kuanza kwa mwaka 2025, wastani wa watu 600 kwa siku walifika nchini Uganda, na idadi hiyo inatarajiwa kufikia milioni 2 mwisho wa mwaka huu,” ilisema taarifa hiyo.

Kwa sasa, Uganda ndio nchi pekee iliyopokea wakimbizi wengi zaidi barani Afrika, ikiwa tayari ina jumla ya wakimbizi milioni 1.93.

Kulingana na Mkurugenzi wa Mahusiano ya Nje wa UNHCR Dominique Hyde, misaada ya dharura nchini Uganda itamalizika mwezi Septemba mwaka huu, huku watoto wadogo wakifa kwa utapiamlo na watoto wa kike kunyanyaswa kingono.

“Uganda imefungua milango yake, shule zaka na taasisi za afya. Hili litafanikiwa lakini halitoshi,” alisema Hyde.