Ubalozi wa Uganda nchini Tanzania wafanya jitihada za kumtafuta mwanaharakati Agather Atuhaire

Agather, ni kati ya wanaharakati wanaodaiwa kukamatwa Mei 19, 2025 jijini Dar es Salaam, wakati wakijiandaa kuhudhuria usikilizwaji wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Newstimehub

Newstimehub

22 Mei, 2025

agather 202 main 1

Serikali ya Uganda kupitia ubalozi wake nchini Tanzania umeiandikia barua, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya jinai ya Tanzania (CID), ikitaka kufahamu taarifa za kukamatwa kwa mwanahabari na mwanaharakati wa Uganda, Agather Atuhaire.

Katika barua hiyo ya Mei 22, 2025, Ubalozi wa Uganda nchini Tanzania, unaomba fursa ya kumtembelea Agather, popote alipo, kuzungumza naye na ikibidi kufanya mpango wa kuachiliwa na kurudishwa nchini Uganda.