Ulimwengu

d08dd1d3 2cce 4274 b301 b9d2c18f96b4 1790502690682

Trump akataa pendekezo la Iran la kufungua tena Mlango-bahari wa Hormuz

Rais wa Marekani anasema Iran inataka kufikia makubaliano ya kufungua mlango-bahari huo mara moja kwa sababu “inapata hasara kubwa sana”.

Iran yapendekeza makubaliano na Marekani kufungua Mlango-bahari wa Hormuz ndani ya siku saba

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, aliwaelezea waandishi wa habari nje ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu pendekezo hilo, akisema kuwa Tehran pia itaanza upya mazungumzo yaliyokwama na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia

Korea Kaskazini yasema itaendelea kuzalisha silaha za kinyuklia

Msimamo huo unakuja baada ya Korea Kaskazini kufanya majiribio ya makombora kadhaa, kupima uwezo wake.

Jeshi la Israel lalipua makazi ya mfungwa wa Kipalestina

Mashuhuda walisema kuwa, wanajeshi hao walivamia mji huo na kuanza kushambulia makazi ya Dawas Hassoun, na kusababisha uharibifu mkubwa, siku ya Jumatano jioni.

Afrika

76422aaa 350f 4c2d 97ea d8befc4dfc6b 1790498864993

Marekani kusitisha ufadhili wa sekta ya afya nchini Zimbabwe kufikia mwishoni mwa mwezi wa Septemba

Marekani itasitisha ufadhili wa programu za afya nchini Zimbabwe mwishoni mwa mwezi wa Septemba, kufuatia kuvunjika kwa mazungumzo kuhusu makubaliano ya afya yaliyopendekezwa na Marekani, ambayo Zimbabwe iliyakataa

Mwanamke wa kumi apatikana amefariki katika msururu wa mauaji nchini Afrika Kusini

Polisi wa Afrika Kusini walipata mwili mwingine siku ya Jumamosi huko Ekurhuleni, mashariki mwa Johannesburg.

Qatar Airways yakopesha marubani kwa shirika la ndege la taifa la Rwanda

Msemaji wa Qatar Airways alisema kuwa fursa hiyo ya hiari ya kuhamishiwa kazi kwa muda mfupi itatoa fursa muhimu za kupata uzoefu kurusha ndege kwa marubani.

Wapiganaji wa RSF wahamia upande wa jeshi la Sudan baada ya kushuhudia ‘maafa’

Wapiganaji walioasi wanasema uamuzi huo ulifuatia ‘maafa’ yaliyoshuhudiwa ndani ya kundi hilo la wanamgambo.