Somalia inakabiliwa na ongezeko la dondakoo kutokana na uhaba wa chanjo na kupungua misaada

Dondakoo au Diphtheria, ugonjwa wa bakteria unaosababisha kuvimba kwa tezi, matatizo ya kupumua na homa na huathiri zaidi watoto, unaweza kuzuilika kwa chanjo iliyopatikana kwa wingi katikati ya karne ya 20.

Newstimehub

Newstimehub

19 Agosti, 2025

e62c0b41c496456df8eae1176398f368f3c138f87fcb31b158a3b538b071973e

Maambukizi ya ugonjwa wa Dondoakoo au Diphtheria yameongezeka kwa kasi mwaka huu nchini Somalia, ambapo matibabu yameathiriwa na uhaba wa chanjo na kupunguzwa kwa misaada ya Marekani, maafisa wa Somalia walisema.

Zaidi ya maambukizi 1,600, ikiwa ni pamoja na vifo 87, zimerekodiwa, kutoka kesi 838 na vifo 56 katika mwaka wote wa 2024, alisema Hussein Abdukar Muhidin, mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Somalia.

Dondakoo au Diphtheria, ugonjwa wa bakteria unaosababisha kuvimba kwa tezi, matatizo ya kupumua na homa na huathiri zaidi watoto, unaweza kuzuilika kwa chanjo iliyopatikana kwa wingi katikati ya karne ya 20.

Viwango vya chanjo ya watoto nchini Somalia vimeimarika katika muongo mmoja uliopita, lakini mamia ya maelfu ya watoto bado hawajachanjwa kikamilifu.

Bajeti kubwa ya afya inategemea wafadhili

Waziri wa Afya Ali Haji Adam alisema serikali ilijitahidi kupata chanjo ya kutosha kutokana na uhaba wa kimataifa na kwamba kupunguzwa kwa misaada ya Marekani kunafanya iwe vigumu kusambaza dozi ilizokuwa nazo.