Serikali ya Kenya yalalamika kuhusu masharti mapya ya biashara Tanzania

Kenya imewasilisha malalamiko rasmi kuhusu masharti mapya ya biashara na leseni yaliyotangazwa na Tanzania wiki hii.

Newstimehub

Newstimehub

31 Julai, 2025

1753962265569 rjjp9k bd3589c11cef9e821015020f4cf34f394208dc8c9cf05c1ebc199e3c6fd832c8

Kenya inaonya masharti mapya ya kufanya biashara Tanzania na upatikanaji kuwa yanaweza kutatiza uhusiano wa kiuchumi katika kanda na kukiuka misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari waziri wa biashara wa Kenya Lee Kinyanjui ameeleza wasiwasi wake kuhusu sheria ya Fedha 2025 na masharti mapya kuhusu leseni za biashara. Kinyanjui anasema kuongezwa kwa kodi kwa wasiokuwa raia wa Tanzania ni ubaguzi wa kibiashara.

Masharti hayo ya Tanzania yamepiga marufuku kwa wasiokuwa raia kufanya biashara zinazoaminika kuwa ndogo ndogo nchini humo ikiwemo zile za miamala ya pesa, saluni, mikahawa, pamoja na uongozaji wa watalii.

Baadhi ya wafanyabiashara nchini Kenya wamelalamikia hatua hiyo wakiona kama inalenga biashara zao.

Wanaharakati na raia nchini Kenya wametaka serikali yao ilipize kwa kuchukuwa hatua kama hizo dhidi ya raia wa Tanzania.