Rais wa Republic of the Congo, Denis Sassou Nguesso, ameahidi kuboresha uchumi na miundombinu ikiwa atachaguliwa tena.
Rais wa Jamhuri ya Congo Denis Sassou Nguesso ameanza kampeni zake za uchaguzi kwa kuahidi kuboresha miundombinu, kuwekeza zaidi katika sekta ya kilimo na kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.
Katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika Februari 28, alisema kizazi chake kinaweka msingi wa uongozi kwa vizazi vijavyo.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wanakosoa utawala wake wakisema gharama ya maisha na hali ya uchumi imekuwa changamoto kwa muda mrefu licha ya nchi hiyo kuwa na utajiri wa mafuta.
Sassou Nguesso, ambaye amekuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Congo kwa zaidi ya miongo minne, anawania tena urais katika uchaguzi mkuu wa Machi 15, 2026.
CHANZO: Newstimetr














