Rwanda ‘ipo tayari’ kupokea wahamiaji 250 kutoka Marekani

Mpango huo ulisitishwa baada ya uchaguzi wa mwaka jana nchini Uingereza.

Newstimehub

Newstimehub

5 Agosti, 2025

9088950518643e4e441cce52184411a276dabc21771e893dec57e2053cab2d03

Siku ya Jumanne, serikali ya Rwanda ilisema kuwa ipo tayari kuwapokea wahamiaji 250 kutoka nchini Marekani chini ya mpango maalumu ambao haikuwa tayari kuuweka wazi.

Kwa muda mrefu sasa, serikali ya rais Donald Trump imekuwa ikisukuma ajenda ya kuwarudisha Waafrika makwao, wakiwemo watokao Sudan Kusini na Eswatini.

Mpango huo unafuatiwa ule wa awali ambao ulikwama, ukihihusisha Uingereza, ambapo Rwanda ilikubali kupokea wahamiaji haramu kutoka Uingereza.

Hata hivyo, mradi huo ulisitishwa baada ya uchaguzi wa mwaka jana nchini Uingereza.

“Rwanda imekubaliana na serikali ya Marekani kuhusu kupokea wahamiaji 250,” msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo, aliiambia AFP.

Kulingana na Makolo, Rwanda imekubaliana na Marekani kuhusu mpango huo “kwa sababu kila raia wa Rwanda amewahi kukutana na madhila ya kuhamishwa hapo awali “.

Aliongeza kuwa, wote watakaofika Rwanda, watapatiwa mafunzo, huduma ya afya na malazi.