Rais wa Uganda afanya ziara Misri, maongezi kuhusu mto Nile yatarajiwa kufanyika

Ziara yake ni ya kidiplomasia inayolenga kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kuendeleza ushirikiano wa kikanda kwenye Mto Nile.

Newstimehub

Newstimehub

12 Agosti, 2025

1754996323705 0jdn5 dbbfee8536986030640d521d76f2ac498686522fffb2beaefdf4cbcb1ce50a9c

Rais wa Uganda Yoweri Museveni yupo jijini Cairo nchini Misri tangu Agosti 11, 2025, katika ziara rasmi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi.

“Nimefika katika nchi yetu ya kindugu ya Misri kwa mwaliko wa Mheshimiwa Abdel Fattah el-Sisi. Ninatazamia kushirikiana naye juu ya njia za kukuza uhusiano wetu wa nchi mbili,” Rais Museveni alisema katika taarifa mtandaoni.

Ziara yake ni ya kidiplomasia ikilenga kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kuendeleza ushirikiano wa kikanda kwenye Mto Nile.

Misri na Uganda zina Mto Nile ambao Misri unauangalia kama msingi wa uhai wake.

Ziara hiyo inajiri chini ya wiki moja baada ya Museveni kuwa mwenyeji wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Dkt. Badr Abdellaty, katika Ikulu ya Entebbe kwa majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu maendeleo ya Mto Nile.

Wakati na mazungumzo Entebbe, Museveni alisema changamoto kubwa zaidi ya Mto huo sio migogoro ya kijiografia, lakini uharibifu wa mazingira na maendeleo duni katika nchi zinazopakana na mto.