Rais Touadera amualika Putin wa Urusi kutembelea Jamhuri ya Afrika ya Kati

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera, amemualika Rais wa Urusi Vladimir Putin kutembelea nchi yake, shirika la habari la serikali la Urusi TASS liliripoti siku ya Jumatano.

Newstimehub

Newstimehub

7 Januari, 2026

786866935b2502d34ade9e77d472b554e27e20c10be90c04136f4b4d3427db7f

Rais mpya aliyechaguliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera, amemualika Rais wa Urusi Vladimir Putin kutembelea nchi yake, hirika la habari la serikali la Urusi TASS liliripoti siku ya Jumatano.

Urusi wamekuwa mshirika wa Touadera katika miaka ya hivi karibuni, huku 2018 CAR ikiwa nchi ya kwanza ya Afrika Magharibi na Kati kuwaleta mamluki wa Urusi Wagner kwa lengo la kukabiliana na makundi kadhaa ya waasi.

Touadera, aambaye amekuwa madarakani tanu 2016, alishinda muhula wa tatu, matokeo ya awali yalionesha wiki hii, na kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais uliofanyika Disemba 28.

Katika mahojiano kwa njia ya video na TASS, Touadera alisema Putin “alikuwa makini” kwa uhusiano na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Maslahi ya Urusi

Akizungumzia matokeo ya awali ya uchaguzi yaliomuonesha Touadera anaongoza, kundi la liliandika kwenye mtandao wa Telegram: “Hatuna shaka njia iliyochaguliwa ya kuhakikisha utulivu na amani itakuwa sawa.”

Ushindi wa Touadera unatarajiwa kuendeleza sera ya maslahi ya Urusi katika taifa hilo, ikiwemo uchimbaji dhahau na almasi.