Raila Odinga amtaka Rais Ruto kutoa fidia kwa waliouawa wakati wa maandaman ya Gen Z Kenya

Raila, ambaye ni kiongozi wa upinzani na Waziri Mkuu wa zamani, alikua akihutubia umati uliokusanyika kwa maadhimisho ya Madaraka jijini Kisumu Magharibi mwa Kenya.

Newstimehub

Newstimehub

1 Juni, 2025

9cd4c76ec57ae861ff7d9ebe15ef66d9658cdbdeba796decd62ca196988d7ece

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga amemtaka Rais William Ruto kuwafidia familia waliopoteza watoto wao katika maandamano ya Gen Z, yaliyoishia kwa ghasia mwaka jana.

Raila, aliyekuwa akizungumza katika sherehe ya maadhimisho ya Madaraka Day 62, siku ya uhuru wa Kenya, alisisitiza kuwa japo wako kimya kwa sasa, wengi wa waioathiriwa kwa kupoteza wapendwa wao katika maandamano hayo hawajapona machungu hayo.

‘‘Niliona kuwa uliandaa halfa ya maombi na chakula hivi juzi tu, na uliwaomba msamaha waathiriwa wa ghasia za maandamano, hicho ni kitu kizuri maana ndio mwanzo wa upatanisho,’’ alisema Raila. ‘‘ Lakini kuna watu waliojeruhiwa na waliokufa. nataka kukuomba leo kuwa tuwalipe fidia familia waliopoteza wapendwa wao ili tufunge mjadala huu.’’

Raila aliongeza kuwa ni muhimu kwa Wakenya kuishi kwa amani akisisitiza kuwa uwepo wa amani sio tu ukosefu wa vita, bali ni kuwa mwananchi anacho chakula cha kutosha.