Raia wa Rwanda afunguliwa mashtaka Marekani kwa kuhusika na mauaji ya kimbari

Kama inavyodaiwa katika hati ya mashtaka, Faustin Nsabumukunzi aliyeishi Mareknai tangu 2003, alitumia nafasi yake ya uongozi akiwa Rwanda kusimamia ghasia na mauaji ya Watutsi.

Newstimehub

Newstimehub

25 Aprili, 2025

faustin

Mahakama kuu huko New York Marekani imemfungulia mashtaka mwanamume mmoja anayeishia New York kwa kusema uongo juu ya maombi yake ya kadi ya makazi na uraia wa Marekani.

Kitengo cha haki cha Marekani kimesema katka taarifa kwamba alificha jukumu lake la awali kama kiongozi na mhusika wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Kulingana na nyaraka za mahakama, Faustin Nsabumukunzi, 65, wa Bridgehampton, New York, alikuwa kiongozi wa eneo hilo akiwa na cheo cha “Mshauri wa Sekta” nchini Rwanda mwaka 1994 wakati mauaji ya kimbari yalipoanza.

“Kama inavyodaiwa, mshtakiwa alishiriki katika utendajikazi wa vitendo vya kikatili nje ya nchi na kisha akadanganya kwa kutumia kadi ya makazi na kujaribu kupata uraia wa Marekani,” alisema Matthew R. Galeotti, Mkuu wa Kitengo cha Jinai cha Idara ya Haki.

2025 04 07T125849Z 1313305952 RC2XSDA1GJK8 RTRMADP 3 RWANDA GENOCIDE

Kati ya Aprili na Julai mwaka huo, Wahutu walio wengi waliwatesa Watutsi walio wachache, wakifanya vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na mauaji ya kimbari na ubakaji.

Takriban Watutsi 800,000 wa kikabila na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa wakati wa mauaji ya kimbari ya miezi mitatu.

“Haijalishi ni muda gani umepita, Idara ya Haki itatafuta na kuwashtaki watu ambao walifanya ukatili katika nchi zao na kuwaficha ili wapate kuingia na kutafuta uraia nchini Marekani,” Galeotti ameongezea katiak taarifa .

“Kama inavyodaiwa, Nsabumukunzi alidanganya mara kwa mara ili kuficha kuhusika kwake katika mauaji ya halaiki ya Rwanda huku akitaka kuwa mkazi halali wa kudumu na raia wa Marekani,” alisema Mwanasheria wa Marekani John J. Durham wa Wilaya ya Mashariki ya New York.

“Kwa zaidi ya miongo miwili, chini ya uwongo huo aliishi Marekani akiwa na hatia na kufanya starehe ambayo waathiriwa wake hawatawahi kuwa nayo, lakini kutokana na juhudi kubwa za wapelelezi wetu na waendesha mashtaka, mshtakiwa hatimaye atawajibishwa kwa matendo yake ya kikatili, “Durham ameongezea.

Kuhusika katika mauaji ya kimbari

Kama inavyodaiwa katika hati ya mashtaka, Nsabumukunzi alitumia nafasi yake ya uongozi kusimamia ghasia na mauaji ya Watutsi katika eneo lake na kuelekeza makundi ya Wahutu wenye silaha kuwaua Watutsi.

2025 04 14T000000Z 1134855961 MT1 000PN930C RTRMADP 3 AFRICA RWANDA

Anadaiwa kuweka vizuizi barabarani wakati wa mauaji ya halaiki ili kuwaweka kizuizini na kuwaua Watutsi na kushiriki katika mauaji.

Kulingana na majalada ya mahakama, Nsabumukunzi alishtakiwa katika mahakama ya Rwanda licha ya yeye kutokuwepo.

Kama ilivyodaiwa zaidi, Nsabumukunzi aliomba uhamisho wa wakimbizi nchini Marekani mwaka 2003, aliomba na kupokea kadi ya makazi mwaka 2007, na baadaye aliwasilisha maombi ya uraia mwaka 2009 na 2015.

Nsabumukunzi anadaiwa kuwadanganya maafisa wa uhamiaji wa Marekani katika maombi yake ya uhamiaji kwa kukana madai yoyote ya uhamiaji Rwanda, ikiwa ni pamoja na kukana madai yoyote ya uhamiaji, mauaji ya kimbari.

Kitengo cha sheria cha Marekani kinasema kutokana na jitihada zake za kuficha matendo yake wakati wa mauaji ya kimbari, Nsabumukunzi ameweza kuishi na kufanya kazi nchini Marekani tangu mwaka 2003.

Nsabumukunzi anashtakiwa kwa kosa moja la ulaghai wa viza na makosa mawili ya jaribio la ulaghai wa uraia.

Iwapo atapatikana na hatia, anakabiliwa na adhabu ya juu ya kisheria ya miaka 30 jela.