Raia wa Afrika wanaotarajia kuitembelea Burkina Faso, sasa hawatohitaji kulipia gharama za viza.
Hatua hiyo inalenga kukuza muingiliano wa watu na bidhaa ndani ya nchi hiyo, kulingana na Waziri wa Usalama wa Burkina Faso, Mahamadou Sana.
“Kuanzia sasa, raia atokaye nchi yoyote ya Kiafrika, hatolazimika kulipia gharama za viza ili aingie Burkina Faso,” alisema Sana, katika kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré siku ya Alhamisi.