Ni Angola au Kenya mechi ya pili kundi A CHAN 2024?

Paa weusi Angola leo wanaingia uwanjani kutafuta ushindi wao wa kwanza wakati watakapokabiliana na Harambee Stars ya Kenya katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.

Newstimehub

Newstimehub

7 Agosti, 2025

650fca90b2ef2b0ec659ce1e1c87b4167009ad165e745ed9d50a520a82c30264

Kocha wa Harambee Stars Benni McCarthy anasema watakuwa makini wakati watakapokabiliana na Angola kwenye mechi ya kundi ya A, huku wakiwa tayari wametia alama tatu kibindoni.

Timu ya Angola, ambayo iko katika nafasi ya 85 katika orodha ya Shirikisho la Soka duniani FIFA, ikilinganishwa na Kenya, ambayo iko katika nafasi ya 109, na inabidi wakabiliane vilivyo kuepuka wasipoteze fursa ya kufuzu kwa hatua ya muondoano.