Nchi za Afrika zalaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Qatar

Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) ameonya kuwa shambulio hilo linaweza kuathiri hali ambayo tayari ni dhaifu katika Mashariki ya Kati.

Newstimehub

Newstimehub

10 Septemba, 2025

2025 09 10t162313z 1938329254 rc2dogaxw9gl rtrmadp 3 israel palestinians qatar

Nchi za Afrika pamoja na Umoja wa Afrika zimelaani vikali mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel siku ya Jumanne ambayo yalilenga uongozi wa kundi la Wapalestina la Hamas lililoko Qatar, huku zikionya kuwa hatua hiyo imekiuka uhuru wa taifa hilo la Ghuba.

Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) ameeleza kuwa shambulio hilo lina hatari ya kuleta mgogoro mkubwa zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Mahmoud Ali Youssouf alibainisha umuhimu wa Qatar katika upatanishi na diplomasia kwa muda mrefu, na kuomba “mazungumzo mapya kuelekea amani ya haki na ya kudumu katika Mashariki ya Kati.”

Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri pia ilielezea shambulio la Israel kama “ukiukaji wazi wa sheria za kimataifa na uhuru wa taifa.”

‘Mfano wa hatari’

Kairo ilisema shambulio hilo ni “mfano hatari na ongezeko lisilokubalika la mzozo.” Ilionyesha mshikamano kamili na Qatar na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kuzuia mashambulio ya Israel na kuwawajibisha wahusika.

Somalia ilisema mashambulio ya Israel ni “ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa” na tishio kwa amani na usalama wa kikanda na kimataifa.