Mwanasiasa mkongwe nchini Uganda aliye kizuizini, Kizza Besigye alisusia kuanza kwa kesi yake ya uhaini siku ya Jumatatu, akimtuhumu jaji kiongozi kwa upendeleo, wakili wake alisema.
Kuzuiliwa kwa Besigye kwa miezi kadhaa kumeangazia rekodi ya haki za binadamu ya Rais Yoweri Museveni kabla ya uchaguzi wa mapema mwaka ujao ambapo Museveni, 80, anaomba kuchaguliwa tena.
Kesi ya Besigye na msaidizi wake, Obed Lutale, ilitakiwa kuanza kusikilizwa Jumatatu baada ya kuchelewa kwa miezi kadhaa, lakini washtakiwa wote waliamua kususia kusikilizwa kwa kesi hiyo baada ya hakimu, Emmanuel Baguma kukataa kujiondoa, wakili wao Eron Kiiza aliambia shirika la habari la Reuters.
Mawakili wa Besigye walitaja uamuzi wa Baguma wa kumnyima dhamana Besigye kama msingi wa tuhuma za upendeleo.
Msemaji wa mahakama James Ereemye Mawanda alisema hakuna uhalali wa shutuma hizo za upendeleo na kuthibitisha kuwa Baguma alikataa kujiuzulu.
Hakimu Baguma hakupatikana kutoa maoni mara moja.
“Besigye na Lutale walichukua uamuzi wa kutofika mbele ya Jaji Baguma,” wakili Kiiza alisema.