Serikali ya Msumbiji imepokea msaada wa tani 500 za mahindi kutoka Tanzania kufuatia mafuriko yaliyoathiri maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Msaada huo uliwasili Machi 24, 2026 jijini Maputo.
Waziri wa Mipango na Maendeleo wa Msumbiji, Salim Cripton Valá, ameishukuru Tanzania kwa msaada huo, akieleza kuwa ni ishara ya uhusiano mzuri na mshikamano uliopo kati ya mataifa hayo mawili.
CHANZO: Newstimetr














