Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amekataa hatua ya upande mmoja kuhusu Mto Nile, akionya kuwa yeyote anayeamini kuwa Misri itatelekeza haki za maji yake “amekosea.”
Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni, Sisi anasema maji wanayopata kwa mwaka kutoka kwenye vyanzo vyote vya mito ya Nile ni kiwango cha bilioni 1,600, ambayo mengi yanapotea katika misitu, maeneo oevu, na kwenye ardhi.
“Ni kiwango kidogo ambacho kinafika Nile, na hiyo ni Misri na Sudan kwa pamoja wanapata bilioni 85 – ikiwa ni asilimia 4 ya idadi yote,” aliongeza.
Kiongozi huyo wa Misri alisisitiza kuwa kuiachia sehemu yao ya maji “kutamaanisha kuachia maisha ya Misri kabisa,” huku nchi ikikosa njia mbadala ya maji na kuwa na kiwango kidogo cha mvua.