Mgombea Urais aahidi kufuga mamba Ikulu

Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC), jumla ya vyama vya siasa 18 vitashiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, huku vyama 17 vikisimamisha wagombea Urais.

Newstimehub

Newstimehub

9 Septemba, 2025

fdbc6350e3ce87f8f07b6214e1d1705fa61972232aed0c2143d3c39853c6a27d

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Wakulima (AAFP) Kunje Ngombale Mwiru, ameahidi kujenga bwawa la mamba Ikulu, iwapo Watanzania watampa ridhaa ya kuiongoza nchi hiyo.

Akizungumza jijini Morogoro hivi karibuni wakati wa kampeni za kunadi sera zake, Mwiru amesema kuwa kuwa analenga kupambana na mafisadi, ikiwemo kupambana na kukomesha vitendo vya kifisadi nchini Tanzania.

“Ndugu zangu, kiama cha mafisadi kinakuja. Mkinachagua tarehe 29, Ikulu yangu kutakuwa na bwawa la kufuga mamba. Ikulu yangu itakuwa na bwawa la kufuga mamba. Huyo mamba ni kwa ajili ya kitanzi cha mafisadi,” alibainisha.