Sehemu ya mlima iliporomoka kutokana na mvua kubwa nje ya mji wa Conakry, makao makuu ya Guinea, na kusababisha maporomoko katika majengo na kuwaua watu wasiopungua 11, mamlaka zilisema siku ya Alhamisi.
Maporomoko hayo yaliyotokea siku ya Jumatano usiku yaliwajeruhi watu wengine 10, na idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka, idara ya huduma za dharura iliongeza.
“Usiku uliopita, ilikuwa kama saa moja usiku mvua ilikuwa inanyesha, na ghafla mlima ukapromoka. Uliangukia katika nyumba moja iliyokuwepo chini ya mlima. Matope yalifukia nyumba. Hakuna aliyenusurika,” alisema Kone Pepe, mkazi wa eneo hilo.
Mvua kubwa