Licha ya kuwa vinara wa mashindano ya barani Afrika wakiwa na mataji kumi, Malkia Strikers wamekuwa hawafanyi vizuri katika jukwaa la Dunia.
Siku ya Jumatano waliishinda Vietnam kwa seti 3-0 (25-23, 25-22, 25-18) kuwafanya wapate ushindi wao wa tatu katika mechi kumi walizocheza mashindano ya Dunia.














