Malawi yapiga marufuku usafirishaji wa mazao kuimarisha usalama wa chakula

Hatua hiyo inafuatia nchi hiyo kukumbukwa na vimbunga vilivyoathiri uzalishaji wa chakula.

Newstimehub

Newstimehub

6 Novemba, 2025

1762457369170 9pehym 8fdbdec858a24354cbeaeb6837c5f7adaafc8b05d94c3db007ff7010b7a723af

Serikali ya Malawi imepiga marufuku usafirishaji nje wa mazao kwa lengo la kukuza usalama wa chakula nchini humo.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii wa nchini Malawi Charity Musonzo alisema kuwa mpango huwa unalenga la kuhuisha usambazaji wa chakula, kudhibiti bei za mazao ya chakula na kulinda uhai wa wananchi wa Malawi wenye kutegema mahindi kama zao lao la chakula.

“Zao la mahindi lipo chini Sheria ya Udhibiti wa mazao, hivyo ni makosa kusafirisha bila ruhusa maalumu,” alisema Musonzo.

Malawi inakabaliana na uhaba mkubwa wa chakula ambao umeathiri takribani watu milioni 4.

Wakati ufunguzi wa mwaka wa bajeti kwa mwaka 2025, Rais Arthur Peter Mutharika aliielezea hali hiyo kama janga la kitaifa akiitaka jumuiya ya kimataifa kutoa msaada.