Mamlaka nchini Ghana zimefanikiwa “kutambua vyema” miili minane ya maafisa wa serikali waliofariki katika ajali ya helikopta ya jeshi siku ya Jumatano na kufanya mazishi ya watwili wao.
Mazishi ya Waziri wa Mazingira, Sayansi na Teknolojia Ibrahim Murtala Muhammed na Naibiu Mratibu wa Usalama Limuna Muniru Mohammed, yalifanyika siku ya Jumapili, Agosti 10, Shirika la Habari la Ghana liliripoti.
Mazishi hayo ya kitaifa yaliyoongozwa na Rais John Mahama yalifanyika Ikulu mjini Accra na viongozi wengine walihudhuria ikiwemo Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio na Mwenyekiti wa ECOWAS kwa viongozi wa Nchi na Serikali.
“Kwa hiyo tubadilishe huzuni hiyo na kuwa kichocheo cha kuchukua hatua. Tuwaenzi, sito kwa kutoa machozi, lakini kwa kukumbuka waliyoyafanya wakiwa hai na kile amacho wamekufia … Walitumikia Ghana kwa moyo wao wote, na ni jukumu letu kuendeleza huduma hiyo,” Mahama alisema wakati wa hafla hiyo.