Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon Anicet Ekane afia kizuizini

Anicet Ekane alikamatwa mwezi Oktoba kwa kosa kwa la ‘uasi’.

Newstimehub

Newstimehub

1 Desemba, 2025

af80a65cf34a1c6faa26175a6ad9f62d2a8d54ab9ce3040571971e29a99fe4b3

Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon, Anicet Ekane amefariki dunia akiwa kizuizini siku ya Jumatatu.

Kwa mujibu wa wakili wake Emmanuel Simh, mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 74, alikuwa akishililiwa na vyombo vya usalama nchini humo toka Oktoba 24 mwaka huu, kwa kosa la uasi.

Kulingana na Simh, Ekane alikuwa amedhoofu kiafya, licha ya kutopewa huduma ya afya akiwa kizuizini.

Kwa upande wake, chama cha Ekane kimeelezea kifo hicho kama “mauaji ya makusudi.

Hata hivyo, Wizara ya Ulinzi wa nchini humo, imesema kuwa mwanasiasa huyo alipoteza maisha kutokana na magonjwa mengine, na kwamba alipokea matibabu kutoka kwenye kituo cha afya cha kijeshi, kupitia ushauri wa madaktari wake binafsi.

“Alikuwa kwa magonjwa mengine sugu, akiwa pia amepokea matibabu kutoka hospitali ya kijeshi,” wizara hiyo ilisema.

Kulingana na wizara hiyo, uchunguzi umeanza ili kubaini chanzo na mazingira ya kifo cha Ekane.

Ekane, ambaye alikuwa kiongozi wa chama cha African Movement for New Independence and Democracy (MANIDEM) alikamatwa pamoja na wanasiasa wengine, wakati wa vurugu zilizotokana na uchaguzi wa hivi karibuni nchini humo.