Watu nane wamepoteza maisha baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kugonga treni ya mizigo nchini Kenya.
Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Naivasha, Anthony Keter ajali hiyo iliyotokea jioni ya Agosti 7, 2025, ilihusisha treni ya mizigo na basi dogo la kampuni ya Kenya Pipeline (KPC).