Jeshi la Nigeria limewaua wapiganaji zaidi ya 100 wa genge la wahalifu katika mashambulizi ya angani na ardhini mwishoni mwa wiki, kulingana na taarifa za Umoja wa Mataifa zilizoonekana na shirika la AFP Jumatatu.
Makundi haya ya wapiganaji yamekuwa yakishambulia wakazi kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria,kuvamia vijiji, kuteka wakazi kwa kutaka kulipwa kikombozi na kuchoma nyumba baada ya kupora.
Mashambulizi haya ya kijeshi katika eneo lenye mapigano jimbo la kaskazini magharibi la Zamfara yalifanyika usiku wa manane Jumapili katika eneo la Bukkuyum, ambapo ndege za kivita kwa ushirikiano na vikosi vya ardhini ziliwashambulia wapiganaji zaidi ya 400 waliokuwa wamekusanyika katika kambi ya msitu wa Makakkari.
Mashambulizi haya ya kijeshi “huenda ikawa ni majibu ya uvamizi wa mara kwa mara wa wapiganaji, hasa utekaji nyara, katika jimbo hilo mwezi uliopita,” taarifa hiyo inasema, ikionesha uhusiano na kupungua kwa harakati za kijeshi hivi karibuni katika jimbo hilo na mashambulizi kadhaa ya wapiganaji.
Siku ya Ijumaa kijiji cha Bukkuyum Adabka kulikuwa na mashambulizi ya wapiganaji na watu kadhaa walitekwa na maafisa wa usalama 13 kuuawa.
Vurugu kuenea