Huduma za Intaneti zarejea tena nchini Tanzania

Samia Suluhu Hassan alitangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais wa Tanzania na kupata muhula mwingine licha ya ghasia zilizoshuhudiwa nchini humu.

Newstimehub

Newstimehub

4 Novemba, 2025

14fa50f5584698e49e9e5dc0e919e70e8b0ccd2292566537f840b3809d814359

Baada ya siku kadhaa za kukosekana kwa mitandao nchini Tanzania, huduma hizo zimerejea saa chache baada ya kuapishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Jumatatu ya Novemba 3, 2025.

Huduma hizo zilizitishwa kufuatia kuibuka kwa vurugu na maandamano yaliyozuka sehemu mbali mbali za nchi hiyo wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.

Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa, huku mali na miundombinu ikiharibiwa wakati wa vurugu wa za baada ya uchaguzi huo.

Samia Suluhu Hassan alitangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais wa Tanzania na kupata muhula mwingine licha ya ghasia zilizoshuhudiwa nchini humo.

Samia alipata asilimia 98 ya kura katika uchaguzi huo, kulingana na Tume Huru ya Uchaguzi nchini Tanzania INEC.