Hospitali ya Recep Tayyip Erdoğan: Daraja la afya na undugu nchini Somalia

Hospitali hii pia imekuwa daraja katika safari ya Somalia kuelekea ustawi wa kudumu, ikipiga jeki ufufuaji wa mfumo dhaifu wa afya uliodorora kwa miongo kadhaa kutokana na vita vya ndani na miundombinu dhaifu na isiyotosha.

Newstimehub

Newstimehub

11 Septemba, 2025

0832df1bd2f09cd75c8b41d98a5d76e3f1fbaa109364d7856d782bec2857a3be

Tangu ilipoanzishwa mwaka wa 2015 katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, pindi ujenzi wake ulioanza mwaka 2012 ulipokamilika, Hospitali ya mafunzo na utafiti ya Recep Tayyip Erdoğan, iliyopewa jina la Rais wa Uturuki, imekuwa kivutio cha raia wa Somalia.

Hii leo, hospitali hiyo inatoa huduma za matibabu kwa takriban wagonjwa 40,000 kila mwezi wanaotoka sehemu mbalimbali ikiwemo ndani ya Somalia na hata kutoka mataifa jirani kama Kenya, Uganda na Ethiopia.

Ikiwa mojawapo ya hospitali kubwa zaidi nchini Somalia, moja ya vituo vikuu vya afya Afrika Mashariki, na mradi mkubwa zaidi wa kibinadamu wa afya nje ya Uturuki, Hospitali ya Recep Tayyip Erdoğan imetambulika kama ishara inayoonekana zaidi ya udugu kati ya Uturuki na Somalia.

Kwa Wasomali, ni zaidi ya hospitali, na chemchemi ya imani na matumaini.

Ikiwa na uwezo wa vitanda takribani 250, hospitali imejengwa kwa vifaa vya kisasa vinavyojumuisha huduma za dharura, wagonjwa mahututi, vyumba nane za upasuaji, vitengo vya uzazi, kitengo cha kutibu majeraha ya moto, kitengo cha kusafisha damu (dialysis), na idara ya uchunguzi wa mishipa ya damu (angiography).

Hospitali hii pia imekuwa daraja katika safari ya Somalia kuelekea ustawi wa kudumu, ikipiga jeki ufufuaji wa mfumo dhaifu wa afya uliodorora kwa miongo kadhaa kutokana na vita vya ndani na miundombinu dhaifu na isiyotosha.

Daktari Mkuu, Dr. Ibrahim Agaoglu, amesisitiza kuwa lengo la hospitali sio la kibiashara. “Madhumuni halisi ya hospitali hii ni kutoa huduma za afya za kiwango cha juu bila gharama au kwa gharama nafuu zaidi kwa wanaohitaji.

Hospitali hii inatoa huduma bora na za kipekee katika nyanja nyingi nchini.”Ameongeza: “Kwa msaada wa Rais wetu, hospitali hii siyo tu kituo cha huduma za afya, bali pia inawakilisha udugu kati ya watu wa Somalia na Uturuki. Hili ni wazi katika kila nyanja – kuanzia usimamizi hadi wafanyakazi wote. Tunatoa huduma kupitia juhudi za pamoja za wafanyakazi wa Kisomali na Kituruki. Kwa sasa, tunao madaktari wa Kisomali wapatao 170, madaktari wa Kituruki wapatao 30, jumla ya wafanyakazi wa Kisomali 1,040 na wafanyakazi wa Kituruki 80.”Hospitali pia limesifika kwa mchango wake wa utoaji wa elimu ya afya.

Kila mwaka, mamia ya madaktari, wauguzi na wahudumu wa afya wa Kisomali hupokea mafunzo na uzoefu wa vitendo pamoja na wataalamu kutoka Uturuki. Hili ni jambo la kimkakati katika kusaidia Somalia kukuza nguvu kazi yake ya kitabibu, kama alivyofafanua Daktari Agaoglu.“Hospitali yetu ndio hospitali ya pekee ya kigeni ambapo taifa moja linawafundisha madaktari wa taifa jingine.