Hofu imeongezeka nchini Kenya baada ya taarifa kuwa baadhi ya wauzaji wa mafuta wanaanza kuhifadhi bidhaa hiyo wakitarajia kupanda kwa bei katika mwezi ujao. Hatua hiyo inahusishwa na mzozo wa Mashariki ya Kati uliosababisha usumbufu mkubwa wa usambazaji wa mafuta duniani.
Kenya, ambayo hutegemea mafuta kutoka Mashariki ya Kati, imeathirika moja kwa moja na hali hiyo, huku viongozi wa sekta hiyo wakionya kuwa uhaba unaweza kuongezeka iwapo hali ya vita itaendelea.
CHANZO: Newstimetr














