Sekta ya maua nchini Kenya inakabiliwa na hatari ya kuporomoka zaidi huku vita vya Mashariki ya Kati vikisababisha usumbufu mkubwa katika soko la kimataifa. Baadhi ya mashamba yameripoti kushuka kwa mauzo kwa zaidi ya nusu, huku kiasi kikubwa cha maua kikiharibika kutokana na kukosa soko.
Wataalamu wanaonya kuwa iwapo hali hii itaendelea, inaweza kusababisha kupotea kwa ajira kwa maelfu ya watu wanaotegemea sekta hiyo, huku serikali ikishauriwa kuanzisha njia mbadala za usafirishaji ili kuokoa hali hiyo.
CHANZO: Newstimetr














