Ethiopia yakana kufadhiliwa na Marekani ujenzi wa bwawa la umeme

Kulingana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, bwawa hilo lilijengwa kwa kutumia fedha za ndani za nchi hiyo.

Newstimehub

Newstimehub

3 Februari, 2026

3b9ae9c981d8c3377b7864570a68f0d30a2a1297336aef1aabe45b542338451c

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema kuwa nchi yake haikupokea “senti” yoyote kutoka nchi yoyote ya nje, ili kufanikisha ujenzi wa bwawa la kufua umeme, maarufu kama Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD), akipinga madai ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuwa Marekani iliyofadhili mradi huo.

Akihutubia bunge la nchi hiyo, Abiy alisema kuwa ujenzi wa bwawa hilo, ulitekelezwa na vyanzo vya ndani vya Ethiopia.

Bwawa hilo, ambalo limejengwa kwenye mto Nile karibu na mpaka wa Sudan, ndiyo bwawa kubwa la kufulia umeme kwa sasa barani Afrika.

Akizungumza ndani ya Ikulu ya Marekani mwishoni mwa mwezi Januari, Trump alihoji ni kwa nini serikali ya Marekani ilifadhili mradi huo, madai yaliyopingwa na Ethiopia.

Abiy aliongeza kuwa, Ethiopia inakamilisha mradi mwingine wa ufuaji umeme katika mto Omo, utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha gigawati 6,460 za umeme kwa mwaka.