Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema serikali yake inaendelea kufanya juhudi za kidiplomasia ili kusimamisha mapigano yanayoendelea Mashariki ya Kati.
Akizungumza katika mkutano wa wabunge wa chama chake, Erdogan alisema Ankara inalenga kuhakikisha mapigano yanakoma na mazungumzo yanaanza tena.
Alisisitiza kuwa Uturuki iko upande wa amani na inaendelea kushirikiana na mataifa mbalimbali ili kuzuia vita hivyo kuenea katika eneo lote la Mashariki ya Kati.
Rais huyo pia aliikosoa serikali ya Israel akisema hatua zake zinaweza kuongeza mvutano na kuleta athari kubwa katika kanda.
CHANZO: Newstimetr














