DRC yatangaza mlipuko mwingine wa Ebola, watu 15 wafariki

Maambukizi 28 yameripotiwa katika mkoa wa Kasai, huku vifo vikiwa asilima 57 vilivyothibitishwa na taasisi ya utafiti ya kitaifa, amesema Waziri wa Afya Roger Kamba

Newstimehub

Newstimehub

4 Septemba, 2025

899f47506a8f22f15467513a7466a3be26e415ea6a3a33d52176c86af72177cc

Mlipuko wa Ebola umesababisha vifo vya watu 15, ikiwemo wafanyakazi wanne wa afya, katika eneo la Mweka mkoa wa kusini wa Kasai, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waziri wa afya alitangaza Alhamisi, ikiwa ni mlipuko wa 16 wa virusi hivyo katika kipindi cha miongo mitano iliopita.

“Kwa niaba ya Wizara ya Afya, Natangaza rasmi kuzuka tena kwa ugonjwa wa Ebola, ule aina ya Zaire, katika eneo la Boulape, Mkoa wa Kasai,” Waziri wa Afya Roger Kamba aliwaambia waandishi wa habari.

Kamba alisema maambukizi 28 yameripotiwa kufikia sasa, huku asilimia 57 ya vifo vikithibitishwa na taasisi ya utafiti ya kitaifa.

Takwimu hizi ni za muda huku uchunguzi ukiendelea, lakini matokeo zaidi yanatarajiwa hivi karibuni, aliongeza.

Waziri huyo alisema serikali imeanzisha vituo vya dharura kushughulikia hilo.