Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wanamgambo wa M23 wameanza tena mazungumzo ya amani huko Doha, mpatanishi wa kutoka Qatar alisema Jumanne, kufuatia ripoti za ghasia katika eneo la mashariki mwa DRC.
“Tumezipokea pande zote mbili hapa Doha kutoka DRC na M23” kujadili utekelezaji wa makubaliano ya awali, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed al-Ansari aliambia mkutano wa habari.
Serikali ya Congo na M23 walitia saini makubaliano ya kusitisha mapigano mjini Doha mwezi Julai yenye lengo la kukomesha kabisa mapigano ambayo yameharibu eneo la mashariki mwa DRC lenye utajiri wa madini.
Chini ya masharti ya makubaliano hayo, pande hizo mbili zilipaswa kuanza mazungumzo ya amani Agosti 8 na kukamilisha makubaliano ifikapo Agosti 18, hata hivyo makataa yote mawili yameisha.
‘Kubadilishana kwa wafungwa’